Tunatoa msaada na kupendekeza kutumia vifaa vifuatavyo:
Mara tu unapokuwa na moja ya vifaa hivi, sakinisha WhatsApp na uthibitishe namba yako ya simu. Kumbuka ya kwamba WhatsApp inaweza kuamilishwa na namba moja ya simu kwenye kifaa kimoja kwa wakati mmoja tu. Zaidi ya hayo, hakuna hiari ya kuhamisha historia yako ya soga kati ya majukwaa. Hata hivyo, tunatoa fursa ya kusafirisha historia ya soga kama kiambatisho cha barua pepe. Jifunze jinsi ya kusafirisha historia ya soga kwenye: Android | iPhone | Windows Phone
Kwa mifumo inayofuata ya uendeshaji, huwezi tena kuunda akaunti mpya, wala kurejesha tena akaunti zilizopo. Hata hivyo, utakuwa na uwezo wa kuendelea kutumia WhatsApp:
Hutaweza kutumia mifumo yote ya uendeshaji wa Windows Phone baada ya Desemba 31, 2019, na WhatsApp inaweza kuwa haitapatikana kwenye Duka la Microsoft baada ya Julai 1, 2019.
Kumbuka: Kwa sababu hatuendelezi kikamilifu mifumo hii ya uendeshaji, baadhi ya vipengele vinaweza kuacha kufanya kazi wakati wowote.