Jinsi ya kuthibitisha namba ya simu
Ni lazima uthibitishe namba yako ya simu ili kuanza kutumia WhatsApp.
Kuthibitisha namba ya simu:
- Fungua WhatsApp.
- Bonyeza Masharti & Faragha kusoma Masharti ya Huduma na Sera za Faragha.
- Bonyeza Kibali kukubali Masharti na endelea.
- Bonyeza Chagua nchi.
- Tafuta nchi au chagua nchi yako na bonyeza CHAGUA NCHI.
- ingiza namba yako ya simu.
- Bonyeza Msaada ikiwa unataka kuzuru Kituo cha Msaada au Wasiliana nasi.
- Bonyeza Mbele > SAWA kupokea msimbo wa uthibitishaji kwa SMS.
- Ingiza msimbo wa tarakimu-6 kutoka kwa SMS.
- Ikiwa hukupokea msimbo, unaweza kubonyeza Tuma tena SMS au Nipigie simu kupigiwa simu na mfumo wa kiotomatiki ili kupewa msimbo.
- Ingiza jina lako. Tafadhali kumbuka:
- Kikomo cha jina ni herufi 25.
- Unaweza pia kuongeza Picha ya Jalada.
- Bonyeza Imekamilika.
Kumbuka: Video ifuatayo inawahusu tu watumiaji wa WhatsApp ambao wana JioPhone au JioPhone 2.