Ikiwa hauwezi kutuma au kupokea jumbe kwenye WhatsApp labda haujaunganishwa kwenye Intaneti. Kutatua matatizo:
- Angalia kama kuna ikoni ya saa karibu na jumbe za badala ya alama ya usahihi. Ikiwepo, basi jumbe zako hazitumwi.
- Angalia ishara ya mtandao kwenye simu yako na uone ikiwa ina mwekamweka mara kwa mara au haipo.
Labda sio lazima kufuta na kusakinisha upya WhatsApp. Mengi ya matatizo ya muunganisho yanaweza kusuluhishwa kwa kufanya yafuatayo:
- Anzisha upya simu yako, kwa kuizima na kuiwasha.
- Angalia kama programu zingine zinafanya kazi. Ikiwa hazifanyi, jaribu muunganisho tofauti wa Intaneti.
- Sasisha WhatsApp kwa toleo la karibuni linalopatikana kwenye duka la programu tumizi ya simu yako.
- Wasiliana na mtoa huduma wako wa simu.
Kumbuka: Video ifuatayo inawahusu tu watumiaji wa WhatsApp ambao wana JioPhone au JioPhone 2.