Jinsi ya kusambaza sasisho la hali
Tumia kipengele cha kusambaza ili usambaze sasisho lako la hali kwa waasiliani wako. Masasisho ya hali yaliyosambazwa hupokelewa kama ujumbe wa WhatsApp.
Kusambaza sasisho
- Fungua WhatsApp > Hali.
- Chagua sasisho la hali unalotaka kusambaza.
- Bonyeza > Sambaza.
- Tafuta au chagua mwasiliani unayetaka au kikundi unachotaka kusambazia sasisho.
- Bonyeza Tuma.