Unaweza kuacha kupokea ujumbe na simu kutoka waasiliani fulani kwa kuwazuia.
Kumzuia mwasiliani
- Bonyeza Hiari > Mipangilio > Akaunti > Faragha > Iliyozuiwa > Ongeza mpya...
- Tafuta au chagua mwasiliani unayetaka kumzuia.
- Bonyeza ZUIA.
Hapa kuna baadhi ya hiari mbadala za kumzuia mwasiliani:
- Chagua soga iliyo na mwasiliani kwenye orodha yako za soga, kisha bonyeza Hiari > Tazama mwasiliani > Zuia > Zuia.
- Fungua soga iliyo na mwasiliani, kisha bonyeza Hiari > Tazama mwasiliani > Zuia > Zuia.
Zuia namba ya simu isiyojulikana
Kuzuia namba ya simu isiyojulikana, kuna hiari mbili:
- Chagua soga iliyo na namba ya simu isiyojulikana kwenye orodha yako aa soga, kisha bonyeza Hiari > Tazama mwasiliani > Zuia > Zuia.
- Fungua soga iliyo na namba ya simu isiyojulikana, kisha bonyeza Hiari > Tazama mwasiliani > Zuia > Zuia.
Dondoo:
- Ujumbe na simu zilizotumwa kutoka kwa mwasiliani aliyezuiwa hazitaonekana kwenye simu yako na hazitatumwa kwako.
- Mwisho kaonwa, mtandaoni, na mabadiliko yoyote yaliyofanyika kwenye picha yako ya jalada hayataonekana tena kwa waasiliani uliowazuia.
- Kumzuia mtu hakutamwondoa mwasiliani kutoka kwenye orodha ya waasiliani, wala hakutakuondoa kutoka kwenye orodha iliyo kwenye simu ya mwasiliani. Kufuta mwasiliani, lazima umfute mwasiliani kutoka kwenye kitabu cha anwani cha simu yako.
- Kama una wasiwasi kuwa mwasiliani aliyezuiwa atajua unamzuia, tafadhali soma makala hii.
Kumruhusu mwasiliani
- Bonyeza Hiari > Mipangilio > Akaunti > Faragha > Iliozuiwa.
- Chagua mwasiliani unayetaka kumruhusu.
- Bonyeza RUHUSU.
Hapa kuna hiari kadhaa mbadala za kumzuia mwasiliani:
- Chagua soga iliyo na mwasiliani kwenye orodha yako ya soga, kisha bonyeza Hiari > Tazama mwasiliani > Ruhusu.
- Fungua soga iliyo na mwasiliani, kisha bonyeza Hiari > Tazama mwasiliani > Ruhusu.
Dondoo:
- Kama ukimruhusu mwasiliani, hutapokea ujumbe wowote au simu zilizotumwa wakati alikuwa amezuiwa.
- Kama ukimruhusu mwasiliani au namba ya simu ambayo haijahifadhiwa hapo awali kwenye kitabu cha anwani cha simu yako, huwezi kumrejesha mwasiliani huyo au namba ya simu kwenye simu yako.