Jinsi ya kuweka au kuondoa nyota kwenye ujumbe
Kipengele cha jumbe zenye nyota kinakuruhusu kuziwekea alama jumbe maalum ili uweze kuzirejea tena baadaye.
Kuweka nyota kwenye ujumbe
- Fungua WhatsApp.
- Kwenye soga ya kibinafsi au kikundi, chagua ujumbe unaotaka kuwekea nyota.
- Bonyeza Hiari > Nyota.
Kuondoa nyota kwenye ujumbe
- Fungua WhatsApp.
- Kwenye soga ya kibinafsi au kikundi, chagua ujumbe unaotaka kufuta.
- Bonyeza Hiari > Ondoa nyota.
Kumbuka: Kuondoa nyota hakutafuta ujumbe.
Kuangalia orodha ya jumbe ulizoziwekea nyota
- Fungua WhatsApp.
- Bonyeza Mipangilio > Jumbe zilizowekwa nyota.