Kama hutaki kuandika ujumbe, unaweza kunakili na kutuma ujumbe wa sauti.
Tuma ujumbe wa sauti
- Fungua soga ya kibinafsi au ya kikundi.
- Hakikisha sanduku la Ujumbe limechaguliwa.
- Bonyeza SAUTI > SAUTI na anza kuzungumza ili kunakili ujumbe wako wa sauti.
- Bonyeza Acha kuacha kunakili.
- Kisha unaweza:
- Kubonyeza Cheza kusikiliza ujumbe wa sauti.
- Kubonyeza TUMA kutuma ujumbe wa sauti.
- Kubonyeza Futa kufuta ujumbe wa sauti.
Dokezo: Unaweza kusubiri kwa sekunde moja kabla ya kuzungumza kama mwanzo wa ujumbe wako haujanakiliwa.
Kwenye ujumbe wa sauti utaona:
- Maikrofoni ya kijani
kwenye ujumbe wa sauti ambao mpokeaji hajaucheza. - Maikrofoni ya bluu
kwenye ujumbe wa sauti ambao mpokeaji ameucheza.
Dokezo: Video hapo chini inawahusu tu watumiaji wa WhatsApp ambao wana JioPhone au JioPhone 2.
Rasilimali zinazohusiana: