Jinsi ya kunyamazisha au kuruhusu arifa za kikundi
Unaweza kunyamazisha arifa za kikundi kwa muda maalum. Bado utapokea ujumbe uliotumwa kwenye soga ya kikundi, lakini simu yako haitatetema au kutoa sauti ujumbe unapopokelewa.
Kunyamazisha arifa za kikundi
- Chagua soga ya kikundi cha WhatsApp.
- Bonyeza Hiari > Nyamazisha > SAWA.
- Chagua muda ambao ungependa kunyamazisha arifa.
- Bonyeza SAWA.
Kurejesha arifa za kikundi
- Chagua soga ya kikundi cha WhatsApp.
- Bonyeza Hiari > Rejesha arifa > SAWA.