Unaweza kufuta jumbe kwako mwenyewe au omba kwamba jumbe zifutwe kwa kila mtu.
Kufuta jumbe kwa kila mtu
Kwa kufuta jumbe za kila mtu kunakukubalia kufuta jumbe maalum ulizotuma kwa soga ya kibinafsi au kikundi. Hii ina faida ikiwa ulituma ujumbe kwa soga isiyo sawa au ujumbe una kosa.
Jumbe ambazo zimefutwa tayari zitawakilishwa na:
“Ulifuta ujumbe huu”
Jumbe zilizofutwa na mtumaji kwa kila mtu zitawakilishwa na:
“Ujumbe huu ulifutwa”
Kufuta ujumbe kutoka kwa kila mtu:
- Kwenye soga ya kibinafsi au kikundi, chagua ujumbe unaotaka kuufuta.
- Bonyeza Hiari > Futa > Futa kutoka kwa kila mtu.
Kumbuka:
- Ili jumbe zifutwe kwa ufanisi kwa kila mtu, wewe na wapokeaji lazima mtumie toleo la karibuni la WhatsApp.
- Wapokeaji wanaotumia WhatsApp ya iOS bado wanaweza kuwa na jumbe zikiwa zimehifadhiwa kwenye picha zao hata baada ya kufutwa kwenye soga za WhatsApp.
- Wapokeaji wanaweza kuona ujumbe kabla haujafutwa au kama ufutaji haukufanikiwa.
- Hautaarifiwa kama ufutaji wa ujumbe kwa kila mtu haukufanikiwa.
- Una saa moja tu baada ya kutuma ujumbe kutimiza Futa kutoka kwa Kila Mtu.
- Kufuta jumbe nyingi kwa mara moja haikuwezeshwa kwenye KaiOS.
Jifutie jumbe
Unaweza kufuta nakili ya jumbe zako ulizotuma au kupokea kwa simu yako. Hii haina athari kwenye soga za wapokeaji wako. Wapokeaji wako bado wataona jumbe katika skrini zao za soga.
Kujifutia jumbe:
- Kwenye soga ya kibinafsi au kikundi, chagua ujumbe unaotaka kufuta.
- Bonyeza Hiari > Futa > Futa kutoka kwangu.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kufuta jumbe: Android | iPhone