Jinsi ya kufuta ujumbe
Unaweza kufuta ujumbe kwako mwenyewe au kuomba ujumbe ufutwe kwa kila mtu.
Kufuta ujumbe kwa kila mtu
Kufuta ujumbe kwa kila mtu hukuruhusu ufute ujumbe mahususi uliotuma kwenye soga ya binafsi au ya kikundi. Hii ni muhimu hasa ikiwa ulituma ujumbe kwenye soga isiyo sahihi au ujumbe uliotuma una makosa.
Ujumbe ambao umefutwa kwa kila mtu utawakilishwa na:
“Umefuta ujumbe huu”
Nafasi ya ujumbe ambao mtumaji ameufuta kwa kila mtu itachukuliwa na:
“Ujumbe huu umefutwa”
Kufuta ujumbe kwa kila mtu:
- Kwenye soga ya binafsi au ya kikundi, chagua ujumbe unaotaka kuufuta.
- Bonyeza Chaguo > Futa > Futa kwa kila mtu.
Kumbuka:
- Ili ujumbe ufutwe kwa kila mtu, wewe na wapokeaji lazima muwe mnatumia toleo la karibuni la WhatsApp.
- Wapokeaji wanaotumia toleo la WhatsApp la iOS bado wanaweza kuwa na maudhui uliyotuma yakiwa yamehifadhiwa kwenye Picha zao, hata baada ya kufutwa kwenye soga ya WhatsApp.
- Wapokeaji wanaweza kuona ujumbe kabla haujafutwa au kama ufutaji haukukamilika.
- Hutaarifiwa kama ufutaji haukufanikiwa kwa kila mtu.
- Una kama saa moja tu baada ya kutuma ujumbe Kufuta kwa Kila Mtu.
- Haiwezekani kufuta ujumbe kadhaa mara moja kwenye KaiOS.
Kujifutia ujumbe
Unaweza kufuta nakala ya ujumbe wako uliotuma au kupokea kwenye simu yako. Hatua hii haina athari kwa soga za wapokeaji wako. Wapokeaji wako bado wataona ujumbe katika skrini zao za soga.
Kujifutia ujumbe:
- Kwenye soga ya binafsi au ya kikundi, chagua ujumbe unaotaka kuufuta.
- Bonyeza Chaguo > Futa > Futa kwangu.