Kipengele cha kuomba taarifa ya akaunti kinakuruhusu kuomba na kuhamisha ripoti ya akaunti yako ya taarifa ya WhatsApp na mipangilio. Ripoti haitakuwa na ujumbe wako. Kama unahitaji kufikia ujumbe wako kando ya kuwa kwenye programu, unaweza kuhamisha historia yako ya soga badala yake.
Kwa kawaida ripoti yako itapatikana baada ya siku tatu baada ya tarehe ulioiomba. Unaweza kurejea kwenye tarehe ambayo Itakuwa tayari unaposubiri ripoti.
Mara unapoomba ripoti, huwezi kutengua au kukatisha ombi lako linalosubiriwa.
Kama ukibadilisha nambari yako ya simu au ukifuta akaunti yako, ombi lako linalosubiriwa litabatilishwa na utahitajika kuomba ripoti nyingine.
Ripoti yako ikiwa tayari kupakuliwa, utapokea arifa ya WhatsApp kwenye simu yako, inayosema “Ripoti ya taarifa za akaunti yako sasa inapatikana”. Skrini ya Omba taarifa ya akaunti kwenye WhatsApp itakuambia una majuma machache kupakua ripoti yako baada ya kupatikana, kabla haijafutwa kutoka kwa seva. Kwa sababu ripoti hii ina taarifa yako, unapaswa uwe makini unapohifadhi, kutuma au kupakia kwa huduma zingine zozote.
Dokezo: Baada ya kupakua ripoti kwenye simu yako, utakua na hiari ya kufuta kabisa nakili ya faili ulilopakua kwenye simu yako kwa kubonyeza Futa ripoti > SAWA kwenye skrini ya Omba habari za akaunti. Kufuta ripoti hakutafuta data yoyote ya akaunti yako ya WhatsApp.
Hutaweza kutazama ripoti ililopakuliwa kwenye WhatsApp. Kutazama ripoti, utahitaji kuunganisha simu yako kwenye kompyuta.
Jinsi ya kuomba taarifa ya akaunti yako