Jinsi ya kuhariri jalada lako
Hariri picha yako ya jalada
- Fungua WhatsApp.
- Bonyeza Chaguo > Mipangilio > Jalada.
- Chagua Picha ya jalada.
- Ikiwa:
- Una picha ya jalada: Bonyeza ZAIDI. Unaweza kuchagua Tazama kutazama picha yako, Hariri kupiga picha mpya kwa Kamera yako au kuchagua picha kutoka kwa Matunzio, au Ondoa kuondoa picha yako.
- Huna picha ya jalada: Bonyeza ONGEZA. Unaweza kupiga picha kwa Kamera yako au kuchagua picha kutoka kwa Matunzio yako.
Hariri jalada lako
- Fungua WhatsApp.
- Bonyeza Chaguo > Mipangilio > Jalada.
- Chagua Jina.
- Bonyeza HARIRI, kisha ingiza jina lako jipya.
- Kikomo cha jina ni herufi 25.
- Bonyeza Hifadhi.
Jina lako la jalada litaonekana kwa watumiaji kwenye vikundi ambao hawajahifadhi maelezo yako ya mwasiliani kwenye vitabu vya anwani vya simu zao.
Hariri taarifa zako
- Fungua WhatsApp.
- Bonyeza Chaguo > Mipangilio > Jalada.
- Chagua Kuhusu.
- Bonyeza HARIRI, kisha ingiza taarifa zako mpya.
- Kipimo cha taarifa zako ni herufi 139.
- Taarifa zako haziwezi kuwa tupu.
- Bonyeza Hifadhi.
Dokezo:
- Unaweza kubadilisha mipangilio yako ya faragha kudhibiti atakayetazama picha ya jalada lako na kuhusu taarifa.
- Kama ukizuia mwasiliani, mtu huyo hataweza kutazama sasisho zozote kwenye picha ya jalada au taarifa zako.
Rasilimali zinazohusiana:
- Jinsi ya kuhariri jalada lako kwenye: Android | iPhone | Web na Desktop
- Jinsi ya kubadilisha mipangilio yako ya faragha
- Jinsi ya kubadilisha mipangilio ya faragha za kikundi