Uhakiki wa hatua-mbili ni kipengele cha hiari ambacho huongeza usalama zaidi kwenye akaunti yako. Ukiwezesha uhakiki wa hatua-mbili, jaribio lolote la kuhakikisha namba yako ya simu kwenye WhatsApp lazima iambatane na PIN ya tarakimu sita uliyoiunda kwa kutumia kipengele hiki.
Kuwezesha uhakiki wa hatua-mbili, fungua WhatsApp > Mipangilio > Akaunti > Uhakiki wa hatua-mbili > Wezesha.
Unapowezesha kipengele hiki, unaweza pia kwa hiari kuingiza anwani yako ya barua pepe. Anwani hii ya barua pepe itawawezesha WhatsApp kukutumia kiungo kupitia barua pepe ili kulemaza uhakiki wa hatua-mbili ukisahau PIN yako ya tarakimu sita, na pia kusaidia kulinda akaunti yako. Hatuhakiki anwani hii ya barua pepe ili kuthibitisha usahihi wake. Tunapendekeza sana kutoa anwani sahihi ya barua pepe ili usifungiwe kutoka kwenye akaunti yako ukisahau PIN yako.
Muhimu: Ukipokea barua pepe ili kulemaza uhakiki wa hatua-mbili, lakini haukuiomba, usibofye kiungo. Mtu anajaribu kuhakiki namba yako ya simu kwenye WhatsApp.
Ikiwa umewezesha uhakiki wa hatua-mbili, namba yako haiwezi kukubaliwa kuhakiki tena kwa WhatsApp kwa muda wa siku 7 baada ya kutumia WhatsApp mwisho bila PIN yako. Kwa hiyo, ukisahau PIN yako mwenyewe, lakini haukutoa barua pepe ili kulemaza uhakiki wa hatua-mbili, hata hutaweza kukubaliwa kuhakiki tena kwa WhatsApp kwa muda wa siku 7 baada ya kutumia WhatsApp mwisho. Baada ya siku hizi 7, namba yako itaruhusiwa kuhakiki tena kwenye WhatsApp bila PIN yako, lakini utapoteza jumbe zote unazosubiri baada ya kuhakiki tena - zitafutwa. Ikiwa namba yako imehakikishwa tena kwenye WhatsApp baada ya muda wa siku 30 za kutumia WhatsApp mwisho, na bila ya PIN yako, akaunti yako itafutwa na mpya itaundwa baada ya kuhakiki tena kwa ufanisi.
Kumbuka: Ili kukusaidia kukumbuka PIN yako, WhatsApp itakuuliza mara kwa mara kuingiza PIN yako. Hakuna hiari ya kulemaza hii bila kulemaza kipengele cha uhakiki wa hatua-mbili.