Kwa nini siwezi kutuma video ndefu kwenye WhatsApp?
Kama ukichagua kutuma video uliyonayo, ina kikomo cha megabaiti 16. Kwa simu nyingi, hii itakuwa sawa na sekunde 90 hadi dakika tatu za video. Kama ukichagua video iliyopo ambayo ni kubwa kuliko 16 MB, basi utakuwa na chaguo la punguza urefu wa video kabla ya kuituma. Ikiwa unajaribu kutuma video uliyopokea awali, tafadhali tumia kitufe cha Sambaza kusambaza video kupitia WhatsApp. Kusambaza ujumbe:
- Fungua soga iliyo na video.
- Gusa na shikilia video.
- Gusa Sambaza.
- Gusa kitufe cha sambaza kilichopo kwenye kona ya chini upande wa kushoto na chagua mpokeaji au wapokeaji wako.
Jifunze zaidi kuhusu media, waasiliani na mahali kutoka makala hii.