Jinsi ya kupiga simu ya video
Kupiga simu ya video kunakuwezesha kuzungumza kwa video na watu unaowasiliana nao kwa kutumia WhatsApp.
Kupiga simu ya video
- Fungua soga ya binafsi ya mwasiliani unayetaka kumpigia simu ya video.
- Gusa Simu ya Video
.
Au, fungua WhatsApp, kisha gusa kichupo cha Simu > Simu Mpya
Kupokea simu ya video
Kama simu yako imefungwa, utapokea arifa ya Simu ya video inaingia... kutoka WhatsApp wakati mtu anakupigia simu ya video. Unaweza:
- Kutelezesha arifa kushoto, kisha gusa Angalia > Kubali.
- Au, unaweza kutelezesha arifa kulia ili ukubali simu.
- Kutelezesha arifa kushoto, kisha gusa Angalia > Kataa.
- Kutelezesha arifa kushoto, kisha gusa Angalia > Ujumbe ili ukatae simu na kutuma ujumbe wa haraka.
Kama hujafunga simu yako, lakini haupo kwenye WhatsApp, utapokea arifa ya Simu ya video inaingia... kutoka WhatsApp wakati mtu anakupigia. Unaweza:
- Vuta arifa chini, kisha gusa Kubali au gusa arifa kukubali simu.
- Vuta arifa chini, kisha gusa Kataa.
- Vuta arifa chini, kisha gusa Ujumbe kukataa simu na kutuma ujumbe wa haraka.
Ikiwa simu yako imefunguliwa na upo kwenye WhatsApp, utaona skrini ya Simu ya video ya WhatsApp wakati mtu anakupigia simu ya video. Unaweza kugusa:
- Kubali
- Kataa
- Nikumbushe, kisha chagua kama unataka kukumbushwa Ndani ya saa 1 au Ninapoondoka.
- Ujumbe kukataa simu na kutuma ujumbe wa haraka.
Kubadili kutoka simu ya video kuwa simu ya sauti
- Ukiwa kwenye simu ya video, gusa Zima Video
, kumfahamisha mwasiliani unayempigia simu kwa video. - Mara tu mwasiliani akizima video yake, simu itabadilishwa na kuwa simu ya sauti.
Kubadili kutoka simu ya sauti kuwa simu ya video
- Ukiwa kwenye simu ya sauti, gusa simu ya video > Badilisha.
- Unayempigia ataona ombi la kubadilisha kuwa simu ya video na anaweza kukubali au kukataa kubadili.
Dokezo: Hakikisha wewe na waasiliani wako mna muunganisho wa intaneti imara mnapopiga au kupokea simu ya video ya kikundi. Ubora wa simu ya video utategemea mwasiliani aliye na muunganisho dhaifu.