Jinsi ya kupiga simu ya kikundi
Simu ya kikundi huruhusu hadi washiriki 32 kupigiana simu ya sauti kupitia WhatsApp bila malipo. Kupiga simu ya sauti hutumia muunganisho wa intaneti wa simu yako badala ya kifurushi chako cha dakika za maongezi. Unaweza kutozwa ada za data. Ukipokea simu ya sauti ya kikundi, skrini inayoingia isemayo Sauti ya WhatsApp... itaonyesha washiriki waliopo kwenye simu na mtu wa kwanza katika orodha atakuwa mshiriki aliyekuongeza. Historia ya simu ya sauti ya kikundi itaonekana kwenye kichupo cha Simu. Unaweza kugusa historia ya simu ili uone wahusika mahususi kwenye simu. Unaweza pia kujiunga na simu ambazo hukujibu iwapo zinaendelea.
Kupiga simu ya sauti ya kikundi
Kupiga simu ya kikundi kutoka kwenye soga ya kikundi
- Fungua soga ya kikundi unachotaka kukipigia simu ya sauti.
- Ikiwa soga yako ya kikundi ina washiriki 33 au zaidi, gusa Simu ya Kikundi
. - Ikiwa kikundi chako cha soga kina washiriki 32 au wachache, gusa Simu ya Sauti
kisha uthibitishe uamuzi wako. Watu saba wa kwanza watakaojibu wanaweza kujiunga na simu, na ni wanakikundi pekee ndio wanaweza kushiriki. - Tafuta watu unaotaka kuwaongeza kwenye simu, kisha gusa Simu ya Sauti
.
Kupiga simu ya kikundi kutoka kwenye kichupo cha Simu
- Fungua WhatsApp, kisha gusa kichupo cha Simu.
- Gusa Simu Mpya
> Simu Mpya ya Kikundi. - Tafuta watu unaotaka kuwaongeza kwenye simu, kisha gusa Simu ya Sauti
.
Kupiga simu ya kikundi kutoka kwenye soga ya binafsi
- Fungua soga ya binafsi na mojawapo ya watumiaji unaotaka kuwapigia simu.
- Gusa Simu ya Sauti
. - Mara baada ya mshiriki kukubali simu, gusa Fungua
> Ongeza Mshiriki. - Tafuta mshiriki mwingine unayetaka kumwongeza kwenye simu kisha gusa Ongeza.
- Gusa Ongeza Mshiriki
kama unataka kuongeza washiriki zaidi.
Kujiunga na simu ya sauti ya kikundi
Kujiunga na simu ya sauti ya kikundi inayoingia
- Utapokea arifa mtu anapokualika ujiunge na simu ya sauti ya kikundi.
- Gusa arifa ili ufungue skrini ya maelezo ya simu.
- Kwenye skrini hii, unaweza kukagua kwanza washiriki wa simu na waalikwa wengine.
- Gusa Jiunge ili ujiunge na simu.
- Ukiwa kwenye simu, gusa Fungua
ili ufungue skrini ya maelezo ya simu. - Gusa Ongeza Mshiriki ili uongeze washiriki zaidi kwenye simu.
- Gusa Piga ili utume arifa kwa watu ambao wameshaalikwa.
Kujiunga na simu ya kikundi ambayo hukujibu
- Fungua WhatsApp, kisha gusa kichupo cha SIMU.
- Ikiwa simu ilianzishwa kutoka kwenye soga ya kikundi, unaweza kujiunga kwa kufungua soga hiyo halafu uguse Jiunge.
- Ikiwa simu inaendelea, gusa simu ambayo ungependa kujiunga nayo. Hatua hii itafungua skrini ya maelezo ya simu.
- Gusa Jiunge.
- Hakikisha kwamba wewe na unaowasiliana nao mna miunganisho mizuri ya Intaneti mnapopiga au kupokea simu za sauti za kikundi. Ubora wa simu utategemea mtu mwenye muunganisho hafifu.
- Ukiwa katika simu ya kikundi, hutaweza kubadilisha simu ili iwe ya video.
- Huwezi kuondoa mhusika wakati wa simu ya kikundi. Mtumiaji atahitaji kukata simu ili kujiondoa kwenye simu hiyo.
- Ingawa inawezekana kuwa kwenye simu ya sauti ya kikundi pamoja na mtu uliyemzuia, huwezi kuongeza anwani ambayo umezuia kwenye simu au mtu aliyekuzuia.
- Upigaji wa simu unapatikana kwenye iPhone zinazotumia iOS 12 au matoleo mapya zaidi.
- Huwezi kufikia namba za huduma za dharura kupitia WhatsApp, kama vile 911 nchini Marekani. Kupiga simu za dharura, unapaswa kufanya mipango ya mawasiliano mbadala.