WhatsApp inahitaji namba ya simu inayofanya kazi ili kuunda akaunti. Ikiwa una matatizo ya kuthibitisha, tafadhali thibitisha yafuatayo:
Baada ya kuingiza namba yako ya simu, tafadhali subiri SMS ipokelewe kwenye simu yako. SMS itakuwa na msimbo wa uthibitisho wa tarakimu 6, ambao unaweza kuingiza kwenye skrini ya uthibitisho kwenye WhatsApp. Msimbo wa uthibitisho ni wa kipekee na hubadilika kila unapothibitisha namba mpya ya simu au kifaa. Tafadhali usikisie msimbo wa uthibitisho kwani unaweza kufungiwa kwa muda.
Kumbuka: Ikiwa una Kifunguo cha iCloud kilichowezeshwa na ulithibitisha namba hii awali, unaweza kuwa ulithibitishwa kiotomatiki bila kutumia msimbo wa SMS.
Ikiwa hukupokea msimbo wako kupitia SMS, mfumo wetu wa kiotomatiki unaweza kukupigia simu na msimbo wako. Tafadhali subiri muda wa dakika tano ili ukamilike na usihariri namba yako kwa muda huu. Baada ya dakika tano, gusa Nipigie.
Kumbuka: Kutegemeana na mtoa huduma wako, unaweza kupata gharama ya SMS na simu.
Ikiwa umefuata hatua hizi na huwezi kupokea msimbo, tafadhali fanya yafuatayo: