Hesabu ya beji haionekani
Hesabu isiyo sahihi kwenye beji ya aikoni ya WhatsApp husababishwa na tatizo kwenye simu yako. Jaribu hatua hizi za utatuzi ili uiweke upya:
- Mwombe mtu akutumie ujumbe mpya wa WhatsApp: Kufanya hivyo kutaweka upya hesabu ya beji kiotomatiki.
- Hakikisha umewasha beji kwenye mipangilio ya iPhone: Nenda kwenye Mipangilio ya iPhone, gusa WhatsApp > Arifa, washa au zima Beji.
- Weka upya mipangilio ya arifa: Nenda kwenye Mipangilio ya WhatsApp, gusa Arifa > Weka Upya Mipangilio ya Arifa.
- Ondoa WhatsApp: Gusa na ushikilie programu, kisha Ondoa Programu > Futa Programu > Futa. Kisha sakinisha WhatsApp upya.