Huwezi kutumia kiandikio kwenye WhatsApp
Vipengele vyote vya kiandikio vinadhibitiwa kabisa na iOS, ikiwa ni pamoja na viandikio vya lugha nyingi, Marekebisho ya kiotomatiki, Angalia Tahajia, na Maandishi tabiri. Vipengele hivi vinaweza kuzimwa au kuwashwa kwenye iPhone Mipangilio > Jumla > Kiandikio. Kama vipengele hivi havifanyi kazi, hili ni tatizo la iOS, sio WhatsApp.
Kama uliongeza kiandikio kingine, unaweza kukipata hiki kwa kugusa aikoni ya dunia iliyopo kwenye kona ya chini ya kiandikio.
Ikiwa unakabiliwa na uandikaji wa polepole, kubadili kiandikio au kuongeza emoji, tafadhali anzisha upya kamusi ya kiandikio kupitia iPhone Mipangilio > Jumla > Weka upya > Weka Upya Kamusi ya Kiandikio.
Kujifunza zaidi kuhusu kiandikio kwenye iPhone yako, tafadhali tembelea tovuti ya Msaada wa Apple.