Hali inakuruhusu kushirikisha maandishi, picha, video na sasisho za GIF zinazotoweka baada ya masaa 24. Ili kutuma na kupokea masasisho ya hali kutoka kwa waasiliani wako, wote wewe na waasiliani wako lazima muwe na nambari za simu za kila mmoja wenu zilizohifadhiwa katika vitabu vyenu vya anwani.
Kuunda na kutuma sasisho ya hali
Fungua WhatsApp > gusa Hali.
Gusa:
Kamera au Hali yangu kupiga picha, kurekodi video au GIF au chagua picha iliyopo, video, au GIF kutoka kwa kichaguzi. Unaweza pia kuongeza manukuu au kuhariri picha, video au GIF, unaweza kujifunza jinsi ya kufanya hivyo kwenye makala haya.
Maandishi kutunga sasisho ya hali ya maandishi. Unaweza kugusa T kuchagua fonti au Rangi kuchagua rangi ya mandharinyuma.
Gusa Tuma.
Mbadala, unaweza kuunda na kutuma picha, video au sasisho za hali za GIF kwa kugusa Kamera.
Kutazama au kujibu sasisho ya hali
Kutazama sasisho ya hali ya mwasiliani, gusa Hali, kisha sasisho ya hali ya mwasiliani.
Kujibu sasisho ya hali ya mwasiliani, gusa Jibuunapokua unatazama.