Kama hatua ya ziada ya usalama kwenye iOS 9 na mpya, unaweza kuwezesha Touch ID au Face ID kwenye WhatsApp. Ikiwezeshwa, ni lazima utumie Touch ID au Face ID kufungua WhatsApp. Unaweza bado kujibu ujumbe kutoka kwa arifa na kujibu simu kama WhatsApp imefungwa.
Ili kutumia Touch ID au Face ID kwa WhatsApp, lazima kwanza uiwezeshe kwenye iPhone Mipangilio.
Dokezo: Kama Touch ID au Face ID hazifungui WhatsApp, unaweza kuingiza msimbosiri wako wa iPhone.