Jinsi ya kuzuia na kuripoti waasiliani
Unaweza kuacha kupokea ujumbe, simu na masasisho ya hali kutoka kwa waasiliani fulani kwa kuwazuia. Pia unaweza kuwaripoti kama unadhani kuwa wanatuma maudhui yanayotatiza au taka.
Kumzuia mwasiliani
- Fungua WhatsApp Mipangilio > Akaunti > Faragha > Waliozuiwa > Ongeza Mpya....
- Tafuta mwasiliani unayetaka kumzuia, kisha gusa mwasiliani.
Unaweza kutumia mbinu hizi mbadala za kuzuia mwasiliani:
- Fungua soga na mwasiliani, kisha gusa jina la mwasiliani > Zuia Mwasiliani > Zuia au Ripoti Mwasiliani > Ripoti na Uzuie, hatua itakayoripoti na kuzuia nambari hiyo.
- Telezesha kushoto soga yenye mwasiliani kwenye kichupo cha Soga yako, kisha gusa Zaidi > Maelezo ya Mwasiliani > Zuia Mwasiliani > Zuia au Ripoti Mwasiliani > Ripoti na Uzuie, hatua itakayoripoti na kuzuia nambari hiyo.
Kuzia nambari ya simu usiyoijua
Ili kuzuia nambari ya simu usiyoijua, una chaguo mbili:
- Ikiwa ni mara ya kwanza umepokea mawasiliano kutoka kwenye nambari hiyo ya simu, unaweza kufungua soga kisha uguse Zuia > Zuia.
- Fungua soga iliyo na nambari ya simu usiyoijua, kisha gusa nambari ya simu > Zuia Mwasiliani > Zuia au Ripoti Mwasiliani > Ripoti na Uzuie, hatua itakayoripoti na kuzuia nambari hiyo.
Kumbuka:
- Waasiliani waliozuiwa hawataweza tena kukupigia simu au kukutumia ujumbe.
- Masasisho yako ya hali, mara ya mwisho kuonwa, kuwa mtandaoni na mabadiliko yoyote unayofanya kwenye picha yako ya jalada hayataonekana tena kwa waasiliani uliowazuia.
- Kumzuia mtu hakutamwondoa mwasiliani huyu kwenye orodha ya waasiliani, wala hakutakuondoa kwenye orodha iliyo kwenye simu ya mwasiliani huyu. Ili ufute mwasiliani, lazima umfute kutoka kwenye kitabu cha anwani cha simu yako.
- Kama una wasiwasi kuwa mwasiliani aliyezuiwa atajua kuwa umemzuia, tafadhali soma makala haya.
Kumruhusu mwasiliani
- Gusa Mipangilio > Akaunti > Faragha > Waliozuiwa.
- Telezesha kushoto kwenye jina la mwasiliani.
- Au, gusa Hariri > aikoni ya alama nyekundu ya kutoa.
- Gusa Ruhusu.
Unaweza kutumia mbinu hizi mbadala za kumruhusu mwasiliani:
- Fungua soga iliyo na mwasiliani > kisha gusa jina la mwasiliani Ruhusu mwasiliani.
- Telezesha kushoto soga iliyo na mwasiliani kwenye kichupo cha Soga zako, kisha gusa Zaidi > Maelezo ya mwasiliani > Ruhusu Mwasiliani.
Kumbuka: Ukimruhusu mwasiliani, hutapokea ujumbe wowote, simu na masasisho ya hali yaliyotumwa kwako na mwasiliani wakati alipokuwa amezuiliwa.
Kuripoti mwasiliani
- Fungua soga kati yako na mtumiaji unayetaka kumripoti.
- Gusa jina la mwasiliani, kisha gusa Ripoti Mwasiliani.
- Gusa Ripoti na Uzuie.
Kumbuka: Mara baada ya kuripoti, WhatsApp itapokea ujumbe wa hivi karibuni uliotumwa kwako na mtumiaji au kikundi ulichoripoti, pamoja na maelezo kuhusu mtagusano wako wa hivi karibuni na mtumiaji aliyeripotiwa.
Kuripoti picha au video ya kutazama mara moja
- Fungua picha au video ya kutazama mara moja.
- Gusa Zaidi
kwenye kona ya chini. - Gusa Ripoti Mwasiliani.
Ili kupata maelezo zaidi kuhusu kutazama mara moja, soma makala haya.