Ili kutumia picha na video zako kwenye WhatsApp, utahitajika kuipatia programu ruhusa kufikia Picha kwenye iPhone yako. Ukikataa kutoa ruhusa ya kutumia picha, utaona tahadhari hii:
Unaweza kutoa ruhusa kwa kubadilisha mipangilio ya faragha ya iPhone yako.
Fungua WhatsApp na sasa utaweza kutumia Picha zako za iPhone ulizonazo kwenye WhatsApp.
Hakikisha kwamba huna vikwazo vyovyote vilivyowekwa kwenye iPhone Mipangilio > Muda wa Skrini. Vinginevyo, unaweza kuhitajika kucheleza na kurejesha simu yako.