Jinsi ya kuunganisha kwenye WhatsApp kutoka kwa programu tofauti
Kuna njia kadhaa za kuifanya programu yako ya iPhone kuingiliana na WhatsApp: viungo vya jumla, mipango ya URL maalum, kushirikisha kiendelezi, na API ya Mwingiliano wa Hati.
Viungo vya jumla
Viungo vya jumla vinapendelewa kama njia ya kuungana na akaunti ya WhatsApp.
Tumia https://wa.me/<number> ambapo <number> ni namba ya simu kamili katika muundo kwa kimataifa. Acha, mabano, vistari, alama ya jumlisha, na sufuri zinazoongoza unapo ongeza namba ya simu katika muundo wa kimataifa.
Mifano:
Tumia: https://wa.me/15551234567
Usitumie: https://wa.me/+001-(555)1234567
Viungo vya jumla vinaweza pia kuwa na ujumbe uliojazwa mapema utaonekana kiotomatiki katika sehemu ya jumbe kwenye soga. Tumia https://wa.m/whatsappphonenumber/?text=urlencodedtext ambapo whatsappphonenumber ni namba ya simu iliyo kwenye muundo kamilifu wa kimataifa URL-encodedtext ni URL ya ujumbe usimbaji uliojazwa mapema.
Mfano: https://wa.me/15551234567?text=I'm%20interested%20in%20your%20car%20for%20sale
Kuunda kiungo kilichojazwa mapema na ujumbe, tumia https://wa.me/?text=urlencodedtext
Mfano: https://wa.me/?text=I'm%20inquiring%20about%20the%20apartment%20listing`
Mpango wa URL Maalum
Kufungua URL ya whatsapp:// kwa kutumia parameta zifuatazo, kutafungua programu yetu na kutachukua hatua maalum.
URL | Parameta | Hufungua |
---|---|---|
programu | - | Programu ya WhatsApp Messenger |
tuma | Kiundaji cha soga mpya | |
maandishi | Ikiwepo, maandishi haya yatajazwa kwenye sehemu ya kuingiza maandishi kwa skrini ya mazungumzo. | |
Lengo-C litasababisha mojawapo ya URL hizi kufunguka kama ifuatavyo:
NSURL *whatsappURL = [NSURL URLWithString:@"whatsapp://send?text=Hello%2C%20World!"]; if ([[UIApplication sharedApplication] canOpenURL: whatsappURL]) { [[UIApplication sharedApplication] openURL: whatsappURL]; }
Hakikisha unaweka mpango wa URL ya WhatsApp kwenye maelezo ya programu yako tumizi Info.plist chini ya kifunguo cha LSApplicationQueriesSchemes ikiwa unataka kujua kama WhatsApp imesanikishwa kwenye iPhone ya mtumiaji kwa kutumia -[UIApplication canOpenURL:].
Shirikisha Kiendelezi
Ilitambulishwa kwa iOS 8.0, Shirikisha Kiendelezi inatoa njia rahisi ya programu yoyote kushirikisha maudhui yoyote na programu zingine zilizosanikishwa kwenye iPhone ya mtumiaji. Sasa hii ndiyo njia inayopendelewa ya kushirikisha maudhui yako kwenye WhatsApp. Kutumia Shirikisha Kiendelezi, unda mfano wa UIActivityViewController na uiweke kwenye programu yako. WhatsApp inakubali aina ya maudhui ifuatayo:
- maandishi (UTI: public.plain-text)
- picha (UTI: public.image)
- video (UTI: public.movie)
- faili za maandishi ya sauti na mziki (UTI: public.audio)
- hati za PDF (UTI: com.adobe.pdf)
- kadi za anwani (UTI: public.vcard)
- URL za wavuti (UTI: public.url)
Mwingiliano wa Hati
Ikiwa programu yako inaunda picha, video, au maandishi ya sauti na ungependa watumiaji wako washiriki media hizi kutumia WhatsApp, unaweza kutumia API ya Mwingiliano wa Hati kutuma media kwa waasiliani na vikundi vya WhatsApp.
WhatsApp Messenger inaweza kushughulikia aina anuwai ya media:
- picha za aina zozote ambazo zinafuatana na public.image (kwa mfano, PNG na JPEG)
- video za aina zozote ambazo zinafuatana na public.movie (kwa mfano, video ya MPEG-4)
- faili za sauti (MPEG-3, MPEG-4, AIFF, AIFF-C na Sauti Msingi tu)
Vinginevyo, ikiwa unataka kuonyesha tu WhatsApp kwenye orodha ya programu (badala ya WhatsApp pamoja na programu zingine zinazofuatana na public/*) unaweza kutaja faili ya moja ya aina zilizotajwa hapo awali zilizohifadhiwa na kiendelezi ambacho ni cha kipekee kwa WhatsApp:
- picha - «.wai» ambazo ni aina za net.whatsapp.image
- video - «.wam» ambazo ni aina za net.whatsapp.movie
- faili za sauti - «.waa» ambazo ni aina za net.whatsapp.audio
Inaposababishwa, mara moja WhatsApp itawasilisha mtumiaji na skrini ya kuchagua mwasiliani/kikundi. Media itatumwa kiotomatiki kwa mwasilian/kikundi iliyochaguliwa.
Habari zaidi kuhusu kushirikisha media kwa WhatsApp, mara moja wasiliana na rasilimali kwenye wavuti ya Wasanidi wa Apple.