Kwenye iPhone, hakuna njia ya kuchagua mwito wowote isipokuwa ule unaopatikana ndani ya WhatsApp. Unaweza kubadilisha mwito wakati programu imefungwa kupitia Mipangilio ya WhatsApp > Arifa. Hapa unaweza kuchagua miito tofauti kwa jumbe, jumbe za kikundi na Simu za WhatsApp.
Kwa iOS 10, iOS 11 na iOS 12 na ushirikiano wa simu za wahusika wa tatu, mwito unaotumiwa kwa simu za WhatsApp ni mdundo uliowekwa kwenye maelezo ya mwasiliani ndani ya programu ya Mwasiliani kwenye simu.
Kuweka mwito wa kipekee kwa simu za WhatsApp kwenye iOS 10, iOS 11 na iOS 12:
Kumbuka: Sauti ya arifa ya kipekee za jumbe zinaweza kuwekwa kwenye Mipangilio ya WhatsApp > Arifa.
Muhimu: Kwa sababu ya kasoro kwenye iOS 10, sauti zako za arifa haziwezi kucheza vizuri mpaka uanzishe upya iPhone yako (bonyeza na ushikilie vitufe vya kuwasha na cha nyumbani kwa sekunde 10).