Tafadhali fuata hatua hizi za kufuta na kusakinisha upya WhatsApp:
- Kabla ya kufuta WhatsApp kutoka kwa simu yako, unaweza kutumia kipengele cha Chelezo za Soga kucheleza jumbe zako.
- Kusakinisha upya WhatsApp:
- Gusa na shikilia ikoni ya WhatsApp kwenye Skrini ya Nyumbani hadi ikoni zianze kuchezeshachezesha.
- Gusa x kwenye kona ya ikoni ya WhatsApp.
- Gusa Futa kuondoa programu tumishi na data zake zote.
- Bonyeza kitufe cha Nyumbani.
- Pakua tena WhatsApp Business kutoka kwa Duka la Programu.
Jifunze jinsi ya kusakinisha upya WhatsApp kwenye: Android