Jinsi ya kuhamisha akaunti yako ya WhatsApp Messenger kuenda kwa WhatsApp Business
Kuhama kutoka kwa WhatsApp Messenger kuenda kwa WhatsApp Business ni haraka, rahisi, na kunaaminika.
Hivi ndivyo unavyofanya:
- Sasisha WhatsApp Messenger na pakua WhatsApp Business kutoka kwa Duka la Programu.
- Fungua WhatsApp Business.
- Soma Masharti ya Huduma ya WhatsApp Business. Gusa Kubali na Endelea kukubali masharti.
- WhatsApp Business hutambua kiotomatiki namba unayotumia katika kwenye WhatsApp Messenger. Kuendelea, gusa hiari ya namba yako ya biashara.
- Ikiwa namba inayoonekana sio namba unayotaka kutumia, gusa TUMIA NAMBA TOFAUTI na pitia njia ya kawaida ya mchakato wa uthibitisho.
- Ingiza msimbo wa tarakimu-6 ya SMS kuthibitisha namba yako.
- Hutahitaji kukamilisha hatua hii ikiwa kifunguo cha iCloud kimewezeshwa na umehakikisha namba hii kwenye simu moja kabla.
- Unda jalada lako la biashara > gusa Imekamilika.
- Unaweza kuendelea kuhariri jalada lako la biashara mara tu akaunti yako ya WhatsApp Business ni amilifu.