WhatsApp ya iPhone inahitaji iOS 10 au matoleo mapya zaidi.
Kwa hali bora ya matumizi, tunapendekeza utumie toleo la hivi karibuni la iOS linalopatikana kwa ajili ya simu yako. Tafadhali tembelea tovuti ya Msaada wa Apple ili upate maelezo kuhusu jinsi ya kusasisha programu ya iPhone yako.
Hatuzuii moja kwa moja utumiaji wa vifaa ambavyo mtumiaji anadhibiti mfumo au vilivyofunguliwa. Hata hivyo, kwa sababu marekebisho haya yanaweza kuathiri utendaji wa kifaa chako, hatuwezi kutoa msaada kwa vifaa vinavyotumia matoleo yaliyorekebishwa ya mfumo wa uendeshaji wa iPhone.