Kuhusu vifaa vinavyoweza kutumika
Mfumo wetu unatumika kwenye iOS 12 au matoleo mapya zaidi, lakini tunapendekeza utumiaji wa toleo jipya zaidi linalopatikana.
Kwa maelezo zaidi kuhusu tunavyochagua ni mfumo upi wa uendeshaji tunaweza kuutumia na kinachotokea ikiwa mfumo wako hautaendelea kutumika, soma makala yaliyo hapa.
Ili upate huduma bora zaidi ya kutumia WhatsApp kwenye iOS:
- Tumia toleo la hivi karibuni la iOS: Tunapendekeza utumie toleo la hivi karibuni la iOS linalopatikana kwa ajili ya simu yako. Tafadhali tembelea tovuti ya Msaada wa Apple ili upate maelezo kuhusu jinsi ya kusasisha programu ya iPhone yako.
- Usitumie vifaa vilivyofunguliwa au vilivyorekebishwa mfumo wa uendeshaji: Hatuzuii waziwazi utumiaji wa vifaa vilivyofunguliwa au vilivyorekebishwa mfumo wa uendeshaji. Hata hivyo, kwa sababu marekebisho haya yanaweza kuathiri utendaji wa kifaa chako, hatuwezi kutoa msaada kwa vifaa vinavyotumia matoleo yaliyorekebishwa ya mfumo wa uendeshaji wa iPhone.
- Simu yako lazima iwe na uwezo wa SMS au kupiga: Ili uweze kuanzisha akaunti mpya ya WhatsApp, simu yako lazima iweze kupokea SMS au simu wakati wa mchakato wa uthibitishaji. Haturuhusu uanzishaji wa akaunti mpya kwenye vifaa vinavyotumia WiFi pekee.
Ili kuendana na maendeleo ya hivi punde zaidi katika teknolojia, mara kwa mara huwa tunaacha kutumia mifumo ya uendeshaji ya zamani ili kuelekeza juhudi zetu katika kufanikisha mifumo mipya zaidi.
Tukiacha kutoa huduma kwa mfumo wako wa uendeshaji, utaarifiwa na kukumbushwa mara kadhaa ili upate kifaa kipya na uendelee kutumia WhatsApp. Pia tutasasisha ukurasa huu mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa toleo jipya zaidi la iOS linalotumika kwenye mfumo wetu limeorodheshwa hapa.
Rasilimali zinazohusiana:
- Kuhusu mifumo ya uendeshaji inayotumika
- Kuhusu vifaa vya Android vinavyoweza kutumika