Unaweza ku kagua msimbo wako wa WhatsApp QR kuongea rafiki au maelezo ya mmoja wa wana familia kwenye WhatsApp.
Kagua msimbo wa WhatsApp QR
Kagua kwa kibinafsi
Fungua WhatsApp > Mipangilio.
Gusa ikoni QR inayo onyeshwa jirani na jina lako.
Gusa Kagua > SAWA.
Shikilia kifaa chako juu ya msimbo wa QR ili kukagua.
Gusa kuongeza Waasiliani.
Unaweza pia kukagua kwa kamera ya WhatsApp:
Fungua WhatsApp > gusa Kamera.
Shikilia kifaa chako juu ya msimbo wa QR ili kukagua.
Gusa kuongeza Waasiliani.
Kwenye iPhone 6s na mpya, unaweza kugusa na kushikilia ikoni ya WhatsApp kwenye skrini ya nyumbani kuona menyu ya haraka. Kisha, gusa Kamera kufungua kamera ya WhatsApp.
Kagua kutoka kwa Picha
Fungua WhatsApp > Mipangilio.
Gusa ikoni QR inayo onyeshwa jirani na jina lako.
Gusa Kagua, kisha gusa ikoni ya Picha iliyopo chini ya skrini.
Chagua msimbo wa WhatsApp QR kutoka kwenye picha zako.
Gusa kuongeza Waasiliani.
Kagua kutoka kwa skrini ya Mwasiliani Mpya
Fungua WhatsApp > gusa Soga Mpya.
Gusa Mwasiliani Mpya > Ongeza kupitia kwa msimbo wa QR.
Shikilia kifaa chako juu ya msimbo wa QR kukagua au gusa ikoni ya Picha chini ya skrini na chagua msimbo wa QR wa WhatsApp kutoka kwa Picha zako.
Gusa kuongeza Waasiliani.
Kagua kutoka kwa kamera ya WhatsApp
Fungua WhatsApp > gusa Kamera.
Gusa ikoni ya Picha iliyopo chini ya skrini.
Chagua msimbo wa WhatsApp QR kutoka kwenye picha zako.
Gusa kuongeza Waasiliani.
Kagua kwenye soga
Fungua WhatsApp na nenda kwa soga ya kibinafsi au ya kikundi.
Gusa ikoni ya kamera.
Gusa ikoni ya Picha iliyopo chini ya skrini.
Chagua msimbo wa WhatsApp QR kutoka kwenye picha zako.