Sioni anwani
Kwa hali bora ya utumiaji, tunapendekeza uruhusu WhatsApp ifikie anwani zako.
Kuruhusu ufikiaji wa anwani zako
- Nenda kwenye Mipangilio
ya iPhone > Faragha. - Gusa Anwani.
- Hakikisha WhatsApp imewashwa.
Ikiwa WhatsApp ina rangi ya kijivu au haionekani katika mipangilio ya faragha, hakikisha huna vizuizi vyovyote vilivyowekwa kwenye
Ukiikataza WhatsApp ruhusa ya kuzifikia anwani kwenye simu yako, bado utaweza:
- Kupokea ujumbe kutoka kwa watumiaji wengine wa WhatsApp na vikundi.
- Kubadili mipangilio ya WhatsApp.
Hutaweza:
- Kuona majina yeyote na utaona tu namba za simu.
- Kuanzisha Vikundi vipya au Orodha mpya za Matangazo.
Kutoonekana kwa anwani
Ikiwa huoni baadhi ya watu unaowasiliana nao kwenye WhatsApp, jaribu yafuatayo:
Kwa anwani za kimataifa:
- Hakikisha kwamba umeweka namba sahihi ya simu katika mfumo kamili wa kimataifa.
Ikiwa watumiaji ambao huwaoni wamehifadhiwa katika akaunti ya Exchange, msimamizi wa akaunti yako anaweza kuwa haruhusu WhatsApp au programu nyngine kufikia anwani zako. Unaweza kusuluhisha hali hii kwa:
- Kunakili anwani zako za Exchange kwenda katika kitabu cha anwani cha simu yako au iCloud.
- Kumwomba msimamizi wako wa TEHAMA afanye WhatsApp iwe programu inayosimamiwa kwenye iPhone yako.
Kumbuka:
- Akaunti za Exchange zinawezekana kuwa ni akaunti za kazi.