Kwa kipengele cha orodha ya tangazo unaweza kutuma ujumbe kwa waasiliani wako kadhaa kwa mara moja. Orodha za tangazo ni orodha zilizohifadhiwa za wapokeaji wa ujumbe ambao unaweza kuwatumia mara kwa mara tangazo za jumbe bila kuwachagua kila mara.
Hii itaunda Orodha mpya ya tangazo. Unapotuma ujumbe kwa orodha ya tangazo, itatuma kwa wapokeaji wote ambao wamehifadhi namba yako kwenye vitabu vya anwani kwenye simu zao. Wapokeaji watapokea ujumbe kama ujumbe wa kawaida. Wakijibu, ujumbe utaonekana kama ujumbe wa kawaida kwenye skrini yako ya Soga. Majibu yao hayatatumwa kwa wapokeaji wengine kwenye orodha ya tangazo.
Kumbuka: Waasiliani tu waliokuongeza kwenye kitabu cha anwani cha simu zao watapokea ujumbe wako wa tangazo. Ikiwa mwasiliani wako hapokei jumbe za matangazo yako, angalia kuhakikisha kuwa wamekuongeza kwenye vitabu vyao vya anwani. Orodha za tangazo ni mawasiliano ya moja-kwa-wengi. Ukitaka wapokeaji washiriki kwenye mazungumzo ya kikundi, unapaswa kuunda soga ya kikundi badala yake.
Mbadala, gusa Hariri, halafu "–" ikoni karibu na orodha unayotaka kufuta > Futa.