Kipengele cha jumbe zenye nyota kinakuruhusu kuziwekea ala jumbe maalum ili uweze kuzirejea haraka tena baadaye.
Weka nyota kwenye ujumbe
- Gusa na shikilia ujumbe unaotaka kuwekea nyota.
- Gusa Nyota.
Ondoa nyota kwenye ujumbe
- Gusa na shikilia ujumbe wenye nyota.
- Gusa Ondoa nyota.
Angalia orodha ya jumbe ulizoziwekea nyota
- Fungua soga binafsi au za kikundi zilizo na jumbe zenye nyota unazotaka kuona.
- Gusa jina la mtu binafsi au soga ya kikundi.
- Gusa Jumbe Zenye Nyota.
Kuangalia jumbe zote zenye nyota, nenda kwa Mipangilio ya WhatsApp > Jumbe Zenye Nyota.