Ujumbe wa sauti ya WhatsApp unakuruhusu kuwasiliana papo hapo na waasiliani na vikundi. Unaweza kuitumia kuwakilisha habari muhimu na nyeti kwa wakati. Kwa hivyo, jumbe zote za sauti hupakuliwa kiotomatiki.
Kutuma ujumbe wa sauti
Fungua soga ya kibinafsi au kikundi.
Gusa na shikilia kinasa sauti na anza kuzungumza.
Unapomaliza, ondoa kidole kwenye kinasa sauti. Ujumbe wa sauti utatumwa kiotomatiki.
Unapokuwa unanakili ujumbe wa sauti, unaweza kutelezesha ili kuisitisha.
Rekodi ujumbe mrefu zaidi wa sauti
Fungua soga ya kibinafsi au kikundi.
Gusa na shikilia kinasa sauti na anza kuzungumza.
Telezesha juu kufunga kurekodi bila kutumia mikono.