Kutuma midia, nyaraka, eneo, waasiliani au viungo vya Vyumba vya Messenger
Fungua soga ya kibinafsi au kikundi.
Gusa Ambatisha. Kisha, gusa:
Kamera ili kupiga picha mpya au video kwa kamera yako. Kumbuka: Video zinazrekodiwa kwa kutumia WhatsApp zina kikomo cha MB16.
Picha & Maktaba ya Video ili kuchagua picha au video kutoka kwa Gombo ya Kamera la iPhone au albamu. Baada ya kuchagua picha au video, gusa Ongeza iliyopo chini upande wa kushoto ili kuchagua picha kadhaa au video kwa mara moja.
Waraka ili kuchagua waraka kutoka kwenye hifadhi yako ya iCloud au programu zingine kama vile Hifadhi ya Google, Dropbox na kadhalika. Kumbuka: Kutuma waraka kunapatikana tu kwa watumiaji wenye iOS 9 na ya baadaye. Ukubwa wa faili unaoruhusiwa ni MB 100.
Mwasiliani ili kutuma maelezo ya mwasiliani. Kwa kawaida, maelezo yote yaliyohifadhiwa katika kitabu cha anwani ya simu ya mwasiliani aliyechaguliwa yatashirikishwa. Gusa vipengee kwenye skrini ya Shirikisha Waasiliani ili kuondoa uteuzi kwenye maelezo ambayo hutaki kushirikisha.
Unaweza pia kuongeza manukuu kwenye picha na video. Badili kati ya picha ili kuongeza manukuu kwa kila moja.
Gusa Tuma.
Unaweza pia kushirikisha viungo kwa Facebook au video za Instagram, na zinaweza kuchezwa ndani ya WhatsApp. Mwoneko awali utajitokeza baada ya kubandika kiungo kwenye soga yako.
Kumbuka: Ili kutuma midia, nyaraka, viungo vya Vyumba vya Messenger, eneo au waasiliani, utahitaji kuruhusu programu kufikia iPhone yako Huduma ya Eneo pa iPhone yako, Waasiliani, Picha na Kamera kwenye iPhone Mipangilio > Faragha.
Sambaza midia, nyaraka, eneo au waasiliani au viungo vya Vyumba vya Messenger
Fungua soga ya kibinafsi au kikundi.
Gusa na shikilia ujumbe unaotaka kusambaza, kisha gusa Sambaza. Unaweza kuchagua ujumbe zaidi ya moja.
Unaposambaza midia, nyaraka, maeneo, waasiliani au viungo vya Vyumba vya Messenger, huhitaji kupakia tena. Ujumbe wote ambao mwanzoni haukutumwa na wewe utaonyeshwa na lebo ya "Ulisambazwa".