Jinsi ya kutuma maudhui
Kutuma maudhui, hati, mahali, au anwani
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
- Gusa Ambatisha
. Kisha, gusa:- Kamera ili upige picha mpya au video kwa kamera yako. Kumbuka: Video zinazorekodiwa kwa kutumia WhatsApp zina kikomo cha MB16.
- Maktaba ya Picha na Video ili kuchagua picha au video kutoka kwenye picha za iPhone yako au albamu. Baada ya kuchagua picha au video, gusa Ongeza
iliyopo chini kushoto ili kuchagua picha au video kadhaa kwa mkupuo. - Hati ili uchague waraka kutoka kwenye hifadhi yako ya iCloud au programu nyingine kama vile Hifadhi ya Google, Dropbox na kadhalika. Kumbuka: Uwezo wa kutuma hati unapatikana tu kwa watumiaji wenye iOS 12 na matoleo mapya zaidi. Ukubwa wa faili unaoruhusiwa ni MB 100.
- Mahali ili kutuma mahali au maeneo ya karibu.
- Anwani ili utume maelezo ya mawasiliano. Kwa kawaida, maelezo yote yaliyohifadhiwa katika kitabu cha anwani cha simu kuhusu aliyechaguliwa yatashirikiwa. Gusa vipengee kwenye skrini ya Shiriki Anwani ili uondoe maelezo ambayo hutaki kuyashiriki.
- Unaweza pia kuongeza maelezo mafupi kwenye picha na video. Badili kati ya picha ili uongeze manukuu kwa kila mojawapo.
- Gusa Tuma
.
Unaweza pia kushiriki viungo kwa Facebook au video za Instagram na zinaweza kuchezwa ndani ya WhatsApp. Mwonekano wa kuhakiki utajitokeza baada ya kubandika kiungo kwenye soga yako.
Kumbuka: Ili kutuma maudhui, hati, viungo, au anwani, utahitaji kuruhusu programu ifikie vipengee vifuatavyo vya iPhone yako, Huduma za Mahali, Anwani, Picha na Kamera kwenye Mipangilio ya iPhone > Faragha.
Kusambaza maudhui, hati, mahali au anwani
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
- Gusa na ushikilie ujumbe unaotaka kusambaza, kisha gusa Sambaza. Unaweza kuchagua ujumbe kadhaa.
- Gusa Sambaza
. - Chagua soga unayotaka kusambazia ujumbe kisha gusa Sambaza.
Unaposambaza maudhui, hati, mahali au anwani, huna haja ya kupakua tena. Ujumbe ambao kwa asili haukutumwa na wewe utakuwa na maandishi "Ulisambazwa".
Kumbuka: Maelezo hayatasambazwa pamoja na maudhui.