Jinsi ya kutuma GIF
Jinsi ya kutuma GIF
Unaweza kutuma GIF kwenye soga za binafsi au za kikundi kwenye WhatsApp.
- Fungua WhatsApp.
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
- Gusa Vibandiko
> GIF. - Kisha, unaweza kugusa:
- Tafuta
kutafuta GIF mahususi. - Hivi karibuni
kuona GIF zako ulizotumia hivi karibuni. - Vipendwa
kuona GIF zako unazozipenda.
- Tafuta
- Chagua na gusa GIF unayotaka kutuma.
- Gusa Tuma
.
Kuongeza GIF kwenye Vipendwa
Unaweza kuongeza GIF kwenye Vipendwa ili uweze kuzipata haraka baadaye.
- Kuweka GIF katika vipendwa kutoka kwenye soga, gusa na ushikilie GIF iliyo katika soga ya binafsi au ya kikundi > gusa Nyota
. - Kuweka GIF katika vipendwa kutoka kwenye menyu ya GIF, gusa na ushikilie GIF > gusa Ongeza kwenye Vipendwa.
Kuondoa GIF kwenye Vipendwa
- Gusa Vipendwa
> gusa na ushikilie GIF > gusa Ondoa kwenye Vipendwa.