Jinsi ya kutuma na kufungua maudhui ya kutazama mara moja
Unaweza kutuma picha au video ambayo itatoweka kwenye WhatsApp baada ya mpokeaji kuifungua na kufunga sehemu ya kuangalilia maudhui. Mara tu akishafunga sehemu ya kuangalilia maudhui, maudhui hayo hayataonekana tena kwenye soga hiyo na hayawezi kutazamwa tena. Picha au video za kutazamwa mara moja haziwezi kuhifadhiwa kwenye Picha au Matunzio ya mpokeaji na hawezi kuzisambaza.
Kutuma maudhui ya kutazama mara moja
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
- Gusa Kamera
ili upige picha au kurekodi video au chagua kutoka kwenye Albamu yako. Au, gusa Ambatisha , kisha gusa: - Kamera ili kupiga picha au video mpya kwa kamera yako. Video zilizorekodiwa kwa kutumia WhatsApp zina kikomo cha MB 16.
- Picha na Maktaba ya Video ili kuchagua picha au video iliyopo kutoka kwenye Picha za iPhone yako au Albamu.
- Gusa 1
. - Gusa Tuma
.
Utaona arifa ya kuwa Imefunguliwa kwenye soga mara baada ya mpokeaji kutazama picha au video hiyo.
Kumbuka: Ili kutuma maudhui, utahitaji kuruhusu WhatsApp ifikie Picha za iPhone yako na Kamera katika Mipangilio ya iPhone > Faragha.
Kufungua maudhui ya kutazama mara moja
- Gusa ujumbe wenye 1
. - Tazama picha au video.
- Telezesha au gusa Nyuma
ili kutoka kwenye sehemu ya kuangalia maudhui.
Utaona arifa ya Imefunguliwa kwenye soga kwa maudhui ambayo tayari umeyatazama. Mara baada ya kufunga sehemu ya kuangalilia maudhui, huwezi kutazama maudhui hayo tena au kuripoti maudhui hayo kwa WhatsApp na hayatahifadhiwa kwenye gombo la kamera yako.
Rasilimali zinazohusiana:
- Kuhusu kutazama mara moja
- Jinsi ya kutuma na kufungua maudhui ya kutazama mara moja kwenye: Android | KaiOS | Web na Desktop
- Jinsi ya kuripoti ujumbe kwenye WhatsApp