Jinsi ya kujibu kutoka kwenye Skrini iliyofungwa
Kujibu ujumbe kutoka kwenye Skrini iliyofungwa:
- Gusa na ubonyeze kwa muda mrefu au ubonyeze kwa uthabiti arifa ya ujumbe ili kibodi itokee.
- Weka jibu lako kisha uguse Tuma.
Kumbuka:
- Kipengele cha jibu la haraka kinapatikana kwenye simu za iPhone 6 na mpya zaidi.
- Huenda ukahitaji kurekebisha Mipangilio yako ya Haptic kwa kwenda kwenye Mipangilio > Ufikivu > Miguso > Haptic Touch > Muda wa Mguso.