Unaweza kutuliza arifa za kikundi kwa muda maalum. Bado utapokea jumbe zinazotumwa kwa soga ya kikundi, lakini simu yako haitatikisika au kupiga kelele zinapopokelewa. Jumbe zinazotumwa kwa soga zilizotulizwa hazitaonyeshwa kwenye idadi ya beji kwenye ikoni ya WhatsApp isipokuwa kama umetajwa au kujibiwa kwenye soga.