Tumia kipengele cha kusambaza ili usambaze ujumbe kutoka kwenye soga ya binafsi au ya kikundi kwenda kwenye soga ya binafsi au ya kikundi. Ujumbe uliosambazwa huashiriwa kwa lebo ya “Ulisambazwa” ili kukusaidia kujua kama rafiki au ndugu yako aliandika ujumbe aliotuma au ikiwa ujumbe huo ulitoka kwa mtu mwingine.
Unaposambaza ujumbe unaweza kushirikisha hadi soga tano kwa wakati mmoja. Ujumbe ukiwa umesambazwa mara nyingi, unaweza tu kusambazwa katika soga moja kwa wakati mmoja.
Kusambaza ujumbe
Kwenye soga ya binafsi au ya kikundi, gusa na ushikilie ujumbe unaotaka kusambaza, kisha uguse Sambaza.
Kusambaza ujumbe kadhaa, unaweza kuchagua ujumbe zaidi baada ya kuchagua ujumbe wa kwanza.
Gusa Sambaza.
Tafuta au chagua soga za binafsi au za kikundi unazotaka kusambazia ujumbe.
Gusa Sambaza.
Kumbuka:
Unaweza pia kusambaza media, mahali, au waasiliani ili usizipakie tena.
Ujumbe wowote unaosambaza ambao si wako mwenyewe utaonekana ukiwa na lebo ya "Ulisambazwa" kwako na kwa kila mpokeaji anayepata ujumbe huo.