WhatsApp inakuruhusu kubinafsisha picha na video zako kwa kuongeza vibandiko, emoji, maandishi, michoro ya mikono na vichujio.
Kumbuka: Vipengele hivi vinapatikana tu kwenye iPhone 5s au mpya na iOS 9 au mpya.
Hariri picha na video
Gusa Ambatisha karibu na sehemu ya maandishi.
Piga picha au video mpya, au chagua picha au video iliyopo kutoka kwenye Gombo ya Kamera.
Anza kuhariri picha yako au video.
Ongeza emoji au vibandiko
Gusa Emoji > Kibandiko au Emoji
Gusa kitu utakachopenda kutumia.
Kusogeza kitu, gusa na shikilia, kisha ikokote.
Kubadilisha ukubwa wa kitu, kifinye na ukipanue kukifanya kikubwa au kidogo.
Kuzungusha kitu, finya na ukizungushe.
Kuongeza maandishi
Gusa Maandishi juu ya skrini.
Andika maandishi yanayotakikana kwenye sehemu ya maandishi.
Kuchagua rangi, telezesha kidole chako juu na chini kwenye kichaguo cha rangi.
Kuchagua aina ya mwandiko, telezesha kidole chako kutoka kwenye kichaguo cha rangi upande wa kulia hadi kushoto. Inua kidole kuthibitisha aina ya mwandiko.
Kubadilisha ukubwa wa maandishi, yafinye na yapanue kuyafanya makubwa au madogo.
Kuzungusha maandishi, finya na ugeuze maandishi.
Chora
Gusa Chora.
Tumia kidole chako ilikuchora michoro.
Kuchagua rangi, telezesha kidole chako juu na chini kwenye kichaguo cha rangi. Unaweza kuchagua rangi kwa kila mstari unaouchora.
Tumia vichujio
Telezesha juu kwenye picha au video.
Chagua kichujio.
Futa hariri na tuma
Kufuta vibandiko, emoji au maandishi, zikokote hadi juu ya skrini kuelekea kwenye takataka na ziachilie. Kufuta michoro, gusa Tendua.