Jinsi ya kuhariri picha na video
WhatsApp inakuruhusu kuweka mapendeleo kwenye picha na video zako kwa kuongeza vibandiko, emoji, maandishi, michoro na vichujio.
Kumbuka: Vipengele hivi vinapatikana tu kwenye iOS 10 au matoleo mapya zaidi.
Kuhariri picha na video
- Gusa Ambatisha
kando ya sehemu ya maandishi. - Piga picha au rekodi video mpya au uchague picha au video iliyopo kwenye Gombo ya Kamera yako.
- Anza kuhariri picha au video yako.
Kuongeza emoji au vibandiko
- Gusa Emoji
> Kibandiko au Emoji - Gusa kipengee ambacho ungependa kutumia.
- Ili usogeze kipengee, kiguse na ukishikilie, kisha kiburute.
- Ili ubadilishe ukubwa wa kipengee, kifinye au ukipanue ili ukifanye kuwa kidogo au kikubwa.
- Ili kuzungusha kipengee, kifinye na ukigeuze.
Kuongeza maandishi
- Gusa Maandishi
katika sehemu ya juu ya skrini. - Andika maandishi unayotaka katika sehemu ya maandishi.
- Ili uchague rangi, telezesha kidole chako juu na chini kwenye kiteua rangi.
- Ili uchague aina ya fonti, gusa Maandishi
. Inua kidole chako ili uthibitishe aina ya fonti. - Ili ubadilishe ukubwa wa maandishi, yafinye au uyapanue ili kuyafanya madogo au makubwa.
- Ili uzungushe maandishi, finya na ugeuze maandishi.
Kuchora
- Gusa Chora
. - Tumia kidole chako ili uchore michoro kwa kidole.
- Ili uchague rangi, telezesha kidole chako juu na chini kwenye kiteua rangi. Unaweza kuchagua rangi ya kila mstari unaouchora.
Kutumia vichujio
- Telezesha kidole juu kwenye picha au video.
- Chagua kichujio.
Kufuta mabadiliko na kutuma
Ili ufute vibandiko, emoji au maandishi, viburute hadi sehemu ya juu ya skrini kuelekea kwenye tupio na uviachilie. Ili ufute michoro, gusa
Baada ya kumaliza kuhariri maudhui, gusa
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kutuma maudhui kwenye iPhone