Unaweza kufuta jumbe kwako mwenyewe au omba kwamba jumbe zifutwe kwa kila mtu.
Kufuta jumbe kwa kila mtu
Kufuta jumbe za kila mtu kunakukubalia kufuta jumbe maalum uliyotuma kwa soga ya kibinafsi au kikundi. Hii ina faida ikiwa ulituma ujumbe kwa soga isiyo sawa au kama ujumbe uliotuma una makosa.
Jumbe ambazo zimefutwa tayari zitawakilishwa na:
“Ujumbe huu ulifutwa”
Kufuta jumbe za kila mtu:
Fungua WhatsApp na nenda kwenye soga iliyo na ujumbe unaotaka kufuta.
Gusa na shikilia ujumbe > chagua Futa kutoka kwenye menyu. Kwa hiari, chagua jumbe zaidi ili kufuta jumbe nyingi kwa mara moja.
Ukiulizwa, gusa Zaidi > chagua Futa kutoka kwa menyu.
Gusa Futa > Futa kutoka kwa Kila Mtu.
Kumbuka:
Ili jumbe zifutwe kwa ufanisi kwa kila mtu, wewe na wapokeaji lazima mtumie toleo la karibuni la WhatsApp.
Wapokeaji wanaotumia WhatsApp ya iOS bado wanaweza kuwa na jumbe zikiwa zimehifadhiwa kwenye picha zao hata baada ya kufutwa kwenye soga za WhatsApp.
Wapokeaji wanaweza kuona ujumbe kabla haujafutwa au kama ufutaji haukufanikiwa.
Hautaarifiwa kama ufutaji kwa kila mtu haukufanikiwa.
Una saa moja tu baada ya kutuma ujumbe kuuliza kutimiza Futa kwa kila Mtu.
Kujifutia jumbe
Unaweza kufuta nakili yako ya jumbe ulizotuma au kupokea kwenye simu yako. Hii haina athari kwenye soga za wapokeaji wako. Wapokeaji wako bado wataona jumbe katika skrini zao za soga.
Kujifutia jumbe: