Dokezo: Ikiwa una soga iliyopo kwenye tab Soga, gusa tu Kikundi Kipya.
Tafuta au chagua waasiliani wa kuongeza kwenye kikundi. Kisha gusa Mbele.
Ingiza mada ya kikundi. Hii itakuwa jina la kikundi ambacho washiriki wote wataliona.
Kikomo cha mada ni herufi 25.
Kwa hiari, ongeza ikoni ya kikundi kwa kugusa ikoni ya Kamera. Unaweza kuchagua Piga Picha, Chagua Picha au Tafuta Mtandaoni kuongeza picha. Ukishaweka, ikoni itaonekana karibu na kikundi kwenye tab ya Soga.
GusaUnda unapomaliza.
Kualika kwa vikundi kwa kupitia viungo
Ukiwa mtawala wa kikundi, unaweza kuwaalika watu kujiunga na kikundi kwa kushirikisha kiungo nao. Kushirikisha kiungo cha mwaliko wa kikundi:
Nenda kwenye soga ya kikundi ya WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
Mbadala, telezesha kikundi upande wa kushoto kwenye tab ya Soga. Kisha gusa Zaidi > Maelezo ya kikundi.
Gusa Alika kwa Kikundi kupitia Kiungo.
Chagua Shirikisha Kiungo, Nakili Kiungo au Msimbo wa QR.
Mtawala anaweza Kuanzisha upya kiungo wakati wowote kufanya kiungo cha awali cha mwaliko batili na kuunda kiungo kipya.
Dokezo: Mtumiaji yeyote wa WhatsApp unaye mshirikishia kiungo cha mwaliko anaweza kujiunga na kikundi, kwa hivyo tumia kipengele hiki tu na watu wanaoaminika. Inawezekana kwa mtu fulani kusambaza kiungo kwa watu wengine, ambao wanaweza kujiunga na kikundi bila ukubali zaidi wa mtawala wa kikundi.