Jinsi ya kuunda na kualika washiriki kwenye kikundi
Unaweza kuunda kikundi cha WhatsApp chenye hadi washiriki 256.
Kuunda kikundi
Nenda kwenye kichupo cha Soga katika WhatsApp.
Gusa Soga Mpya > Kikundi Kipya.
Ikiwa una soga iliyopo kwenye kichupo cha Soga, gusa Kikundi Kipya.
Tafuta au chagua waasiliani wa kuweka kwenye kikundi. Kisha, gusa Inayofuata.
Weka mada ya kikundi. Hili litakua jina la kikundi ambalo washiriki wote wataliona.
Ukomo wa mada ni herufi 25.
Unaweza kuweka aikoni ya kikundi kwa kugusa aikoni ya Kamera. Unaweza kuchagua Kupiga Picha, Kuchagua Picha au Kutafuta kwenye Wavuti ili uweke picha. Ukishaweka, aikoni itaonekana karibu na kikundi kwenye kichupo cha Soga.
Gusa Unda unapomaliza.
Kualika washiriki kwenye vikundi kupitia viungo
Ukiwa msimamizi wa kikundi, unaweza kuwaalika watu kujiunga na kikundi kwa kushiriki nao kiungo. Msimamizi anaweza Kubadilisha kiungo wakati wowote ili kubatilisha kiungo cha mwaliko wa awali na kuunda kiungo kipya.
Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
Au, telezesha kikundi upande wa kushoto kwenye kichupo cha Soga. Kisha, gusa Zaidi > Maelezo ya Kikundi.
Gusa Alika kwenye Kikundi kupitia Kiungo.
Chagua Shiriki Kiungo, Nakili Kiungo au Msimbo wa QR.
Ili ubadilishe kiungo, gusa Badilisha Kiungo > Badilisha Kiungo.
Kumbuka: Mtumiaji yeyote wa WhatsApp unayeshiriki naye kiungo anaweza kujiunga na kikundi, kwa hiyo tumia kipengele hiki na watu unaowaamini tu. Inawezekana mtu akasambaza kiungo kwa watu wengine, ambao wanaweza kujiunga na kikundi bila kuwa na ruhusa ya ziada kutoka kwa msimamizi wa kikundi.