Unaweza kucheleza na kurejesha historia yako ya soga ya WhatsApp ukitumia iCloud.
Kumbuka:
Unaweza kujichelezea soga zako wakati wowote unapotaka.
Nenda kwenye Mipangilio ya WhatsApp> Soga > Chelezo ya Soga > Cheleza Sasa.
Unaweza kutumia uchelezaji wa kiotomatiki, unaoratibiwa kwa kugusa Cheleza Kiotomatiki kisha uchague marudio ya kucheleza.
Kufanya hivyo kutacheleza soga na midia yako kwenye akaunti yako ya iCloud. Unaweza kuchagua kujumuisha au kutojumuisha video kwenye chelezo. Mchakato wa uchelezaji wa iCloud unaweza kuchukua muda kukamilika, kutegemea muunganisho wako wa intaneti na ukubwa wa chelezo.
Ikiwa una wasiwasi kuhusu matumizi ya data ya mtandao wa simu, tunapendekeza ucheleze kwenye iCloud yako kwa kutumia Wi-Fi pekee.
Ikiwa uliwahi kucheleza iPhone yako ukitumia iCloud au iTunes, huenda utaweza kurudisha soga zako za WhatsApp kwa kurejesha iPhone yako kutoka kwenye chelezo ya awali. Kwa maelezo zaidi kuhusu kucheleza na kurejesha iPhone yako, tembelea tovuti ya Msaada wa Apple.
Unaweza kujitumia barua pepe iliyo na historia yako ya soga ikiwa ungependa kuhifadhi soga.
Kumbuka: Ikiwa upo Ujerumani, huenda itakubidi usasishe WhatsApp kabla ya kutumia kipengele cha kuhamisha soga.
Jinsi ya kurejesha historia yako ya soga
Imeshindwa kuunda au kurejesha chelezo ya iCloud