Jinsi ya kuhifadhi nakala kwenye iCloud
Unaweza kuhifadhi nakala na kurejesha historia yako ya soga ya WhatsApp ukitumia iCloud.
Kumbuka:
- Historia ya soga za WhatsApp haihifadhiwi kwenye seva zetu.
- Maudhui na ujumbe unaohifadhi nakili haulindwi kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho wa WhatsApp.
- Hatuna uwezo wa kukurejeshea ujumbe wowote ulioufuta.
Kuhifadhi nakala kwenye iCloud
Kujiwekea nakala mwenyewe
Unaweza kujiwekea nakala ya soga zako wakati wowote unapotaka.
Nenda kwenye Mipangilio ya WhatsApp> Soga > Nakala ya Soga > Hifadhi Nakala Sasa.
Kuweka nakala kiotomatiki
Unaweza kutumia uwekaji nakala kiotomatiki, unaoratibiwa kwa kugusa Uwekaji Nakala Kiotomatiki kisha uchague marudio ya kuhifadhi nakala.
Kufanya hivyo kutahifadhi nakala ya soga na maudhui yako kwenye akaunti yako ya iCloud. Unaweza kuchagua kujumuisha au kutojumuisha video kwenye nakala. Mchakato wa kuweka nakala kwenye iCloud unaweza kuchukua muda kukamilika, kutegemea muunganisho wako wa intaneti na ukubwa wa nakala.
Mahitaji
- Sharti uwe umeingia kwenye akaunti ukitumia kitambulisho cha Apple ambacho huwa unakitumia kufikia iCloud.
- Lazima uwe na iOS 12 au matoleo mapya zaidi na sharti uwe umewasha iCloud Drive.
- Ni lazima kuwe na nafasi ya kutosha kwenye iCloud na iPhone yako. Unahitaji angalau mara 2.05 ya nafasi kwenye akaunti yako ya iCloud na kwenye simu yako kuliko ukubwa kamili wa nakala yako.
Ikiwa una wasiwasi kuhusu matumizi ya data ya mtandao wa simu, tunapendekeza uhifadhi nakala kwenye iCloud yako kwa kutumia Wi-Fi pekee.
Kurejesha kutoka kwenye nakala ya awali
Ikiwa uliwahi kuhifadhi nakala ya iPhone yako ukitumia iCloud au iTunes, huenda utaweza kurudisha soga zako za WhatsApp kwa kurejesha iPhone yako kutoka kwenye nakala ya awali. Kwa maelezo zaidi kuhusu kuweka nafasi na kurejesha iPhone yako, tembelea tovuti ya Msaada wa Apple.
Kuhamisha historia ya soga
Unaweza kujitumia barua pepe iliyo na historia yako ya soga ikiwa ungependa kuhifadhi soga.
Kumbuka: Ikiwa upo Ujerumani, huenda itakubidi usasishe WhatsApp kabla ya kutumia kipengele cha kuhamisha soga.
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi ambayo ungependa kuhifadhi.
- Gusa jina la unayewasiliana naye au mada ya kikundi.
- Gusa Hamisha Soga.
- Chagua iwapo unataka Kuambatisha Maudhui au kutuma barua pepe Bila Maudhui.
- Fungua programu ya Barua pepe. Pia unaweza kugusa Zaidi ili upate chaguo zaidi.
- Weka barua pepe yako kisha uguse Tuma.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kurejesha historia yako ya soga
Imeshindwa kuunda au kurejesha nakala ya iCloud