Siri ni msaidizi wa kibinafsi iliyoundwa ndani ya iOS. Unaweza kuuliza Siri kutuma ujumbe wa WhasApp, kupiga simu ya WhatsApp au kusoma kwa sauti ujumbe wa WhatsApp ambao haujasomwa.
Dokezo: Vipengele hivi vinapatikana tu kwenye iOS 10.3 na vya baadaye.
Kwenye iPhone X, XS, XS Max, na XR unaweza kubonyeza na kushikilia kitufe cha pembeni > Washa Siri.
Tembele tovuti ya Msaada wa Apple kwa habari maalum kuhusu jinsi ya kutumia Siri na jinsi Apple hushughulikia data zilizotumwa kupitia kwa Siri.
Dokezo: Kufungua WhatsApp yenye ujumbe ambao haujasomwa kutaweka upya beji ya arifa. Siri itachukulia hili kama vile hakuna ujumbe ambao haujasomwa na kwa hivyo haiwezi kuusoma kwa sauti.