Jinsi ya kutumia Siri kwenye WhatsApp
Siri ni mfumo wa usaidizi wa binafsi ulioundwa ndani ya iOS. Unaweza kuiuliza Siri itume ujumbe wa WhatsApp, kupiga simu ya WhatsApp au kusoma kwa sauti ujumbe wa WhatsApp ambao hujausoma.
Kumbuka: Vipengele hivi vinapatikana tu kwenye iOS 12 au mpya zaidi.
Kuwasha Siri
- Nenda kwenye Mipangilio
ya iPhone > Siri na Utafutaji > washa Sikiliza "Habari Siri" au Bonyeza Kitufe cha Pembeni cha Siri. - iPhone SE (2020) na iPhone 8 na ya zamani: Washa Bonyeza Mwanzo ili ufikie Siri.
- Sogeza hadi chini kisha uguse WhatsApp.
- Washa Tumia na Siri.
Kwenye iPhone X, XS, XS Max, na XR unaweza kubonyeza na kushikilia kitufe cha pembeni > Washa Siri.
Tembele tovuti ya Msaada wa Apple kwa habari maalum kuhusu jinsi ya kutumia Siri na jinsi Apple hushughulikia data zilizotumwa kupitia kwa Siri.
Dokezo: Kufungua WhatsApp yenye ujumbe ambao hujausomwa kutaweka upya beji ya arifa. Siri itachukulia hili kumaanisha kuwa hakuna ujumbe ambao haujasomwa na kwa hivyo haiwezi kuusoma kwa sauti.